Beki wa Chelsea, Ben Chilwell atakuwa nje ya uwanja hadi Desemba 2023 kufuatia jeraha la misuli ya paja.
Beki huyo wa kushoto alipata tatizo hilo katika dakika za mwisho za ushindi wa Chelsea wa mabao 1-0 dhidi ya Brighton katika Kombe la Carabao Jumatano iliyopita.
Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph, Chilwell huenda akawa nje kwa angalau majuma manane kutokana na jeraha hilo.
Imeripotiwa pia kuwa anaweza kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu zaidi kulingana na mwenendo wa jeraha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliondolewa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki Kombe la Dunia kipindi cha kiangazi mwaka jana kutokana na tatizo la misuli ya paja.
Lakini alirejea kucheza Februari mwaka huu na kurudi katika nafasi yake kwenye kikosi cha Gareth Southgate.
Chilwell alianza katika kikosi cha kwanza England ilipocheza mechi za kufuzu Kombe la Euro 2024 dhidi ya Ukraine mwezi uliopita lakini atakosa mechi zilizobaki za Kundi C.
Beki huyo ambaye ni nahodha chaguo la pili Chelsea amecheza mechi moja ya Ligi Kuu England na hakujumuishwa katika kikosi kilichocheza dhidi ya Fulham, ambapo The Blues ilishinda 2-0 kupitia mabao ya kipindi cha kwanza ya Mykhailo Mudryk na Armando Broja.
Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino alifafanua kuhusu hali ya Chilwell kabla ya mechi hiyo ya London Dabi alisema: “Nadhani ni habari mbaya. Kwa alivyoniambia daktari sio njema.”