Msanii Ben Pol ameamua kumuomba radhi Ali Kiba kufuatia tweet yake iliyozua mgogoro kati ya wasanii hao na kupelekea mashabiki wa Kiba kushusha makombora ya matusi kwa mkali huyo wa ‘Sophia’ katika mtandao wa Instagram.

Akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi cha Jahazi cha Clouds Fm, Ben Pol alimuomba radhi Ali Kiba ambaye alikuwa ndani ya studio muda huo na kukiri kuwa alitereza kwa kuandika tweet hiyo iliyomkwaza. Alisema kuwa yeye ni shabiki wa Ali Kiba ambaye anamzidi kiumri na hata muda aliokaa kwenye tasnia ya muziki.

“Mimi shabiki wa Kiba, moyoni mwangu nina furaha kubwa kuona kwamba tuko sawa kwa sasa,” alisema Ben.

Ben Pol ambaye aliimba wimbo wa ‘Njiwa’ wa Ali Kiba ili kudhihirisha kuwa ni shabiki haswa, alisema kuwa kutofautiana kwao na baadae kupatana huenda kukazaa jambo jema zaidi kati yao.

“Mwenyezi Mungu anakuwaga na mipango yake, hatuwezi jua, pengine hapo mbele kunaweza kuwa na bonge ya collabo,” alieleza Ben Pol.

Naye Ali Kiba alieleza kuwa tayari ameshamsamehe Ben Pol na kwamba tweet yake ilimshtua hata yeye kama ilivyowashtua mashabiki wengine.

“Ben Pol mimi bana kiukweli nilikuwa nimekusamehe toka nilivyokuwa nimeona ile lakini kwasababu nilishtushwa kama watu wengine walivyoshtuka nikajua labda utakuwa umeghafilika, lakini kiukweli mimi nilishtuka nilivyoona vile,” alisema Ali Kiba.

Desemba 17 mwaka huu, Ben Pol alimvaa Ali Kiba kwenye mtandao wa Twitter kwa kumtaja akidai kuwa anadhani anapewa nafasi ya juu zaidi wakati hana uwezo huo, kitu alichodai kinamgharimu.

“Bro @officialalikiba mimi naona kama unakuwa overrated halafu inakugharimu… au haikugharimu?” Ilisomeka tweet ya Ben Pol.

Baada ya muda mfupi, Ali Kiba aliijibu tweet hiyo, “INSHAALLAH Heri @iambenpol asante kwa kunyoosha kidole. Sio makosa yako ni dua inafanya kazi yake #KingKiba.”

Lowassa aanza Kuchunga Ng’ombe, Atoa Neno kwa Watanzania
Adai Kuzuiwa Kupanda Ndege Kwa Sababu Ni Muislam