Msanii wa muziki Bongo anayefanya vizuri na wimbo wake wa Kidume aliyomshirikisha msanii toka Nigeria Chidima, Ben Pol ameshindwa kuendeleza ‘drama’ na kuamua kuweka wazi juu ya uvumi kuhusu mahusiano yake na msanii wa vichekesho Anastazia Kisaveli maarufu kama Ebitoke.

Katika ongea ongea ya Ben Pol amefafanua aina ya mwananmke anayeweza kuwa naye na kusema kuwa anapenda mwanamke anayejiamini katika kila kitu anachokifanya hasa katika kuongea.

Ambapo amesema anapenda mwanamke ambaye anajiamini wakiwa wanaongea au hata wakiwa  wananachat, hii inaweza kuleta maana tofauti kwa mashabiki wa wawili hao.

Ambapo kwa maelezo ya Ben Pol inawezekana ikaeleweka kuwa Ebitoke alikuwa hajiamini akiwa anongea na kuchat na Ben Pol, na hiyo ndio sababu aliyomfanya Ben Pol aanze kumpotezea.

“Endapo nikimpenda msichana sifa kubwa huwa naangalia ‘confidence’ yake pindi tukiwa tunaongea na ku-chat, U-smart, umakini na uharaka katika kujibu vitu ambavyo anaulizwa kwa wakati huo”, amesema Ben Pol.

Ben Pol amefunguka hayo baada ya kupita siku chache tokea aliyekuwa anadaiwa kutoka naye kimapenzi ambaye ni msanii wa vichekesho nchini Anastazia Kisaveli ‘Ebitoke’ kulalamika kwamba hapokelewi simu yake wala kujibiwa ujumbe mfupi pindi amtumiapo Ben..

Barry avunja rekodi ya Ryan Giggs
Rihanna ataja wacheza soka anaowakubali, atamani kuolewa nao