Klabu ya Arsenal inataka kumpa mkataba mpya beki wake, Benjamin William White ‘Ben White’ ambao utakuwa na mshahara maradufu zaidi ya ule ambao anaupokea sasa, na kwa taarifa za ndani zinadai huenda akapewa mara mbili yake.

White mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa anapokea mshahara wa Pauni 120,000 kwa juma ambapo kwenye mkataba mpya anadaiwa kuwa atakunja Pauni 240,000 kwa juma.

Beki huyo wa kimataifa wa England, alijiunga na Arsenal miaka miwili iliyopita kwa dau la Pauni 50 Milioni akitokea Brighton ambapo alisaini mkataba wa miaka mitano inayotarajiwa kumalizika mwaka 2026.

White kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Arsenal na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza michuano yote.

Kutokana na umuhimu wake mabosi wa Arsenal wanataka kumuongeza mkataba mpya beki huyo ili kuzima harakati za baadhi ya timu zilizoanza kumnyemelea na kutaka kumsajili.

Kauli ya Dkt. Tulia yafanyiwa kazi kwa vitendo
Van Dabroek apewa kipaumbele Simba SC