Kiungo kutoka nchini Ghana Thomas Partey amesikitishwa na nafasi yake iliyopunguzwa Arsenal na atafikiria kutaka kuondoka katika klabu hiyo ikiwa mambo hayataimarika kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amekosa kucheza kwa sababu ya jeraha alilolipata kwenye sare ya mabao 2-2 na Fulham mwishoni mwa Agosti, na ameona nafasi yake kama kiungo imekuwa kwenye hati hati baada ya ujio wa Declan Rice.
Partey alianza mechi tatu za kwanza za Arsenal kwenye Ligi Kuu kama beki wa kulia kabla ya kuachwa nje, huku Ben White akiingia kwenye safu ya ulinzi ya kati wakati huo Mikel Arteta akipendelea kuwatumia Rice, Martin Odegaard na Kai Havertz.
Alirejea baada ya kupona jeraha katika ushindi wa kishindo dhidi ya Manchester City kabla ya mapumziko ya kimataifa Oktoba, lakini hakutumika kama mchezaji wa akiba kwenye sare ya mabao 2-2 na Chelsea katika Uwanja wa Stamford Bridge Jumapili (Oktoba 22).
Jorginho alichaguliwa na Arteta kuanza mchezo pale Chelsea kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Emile Smith Rowe na Havertz na Leandro Trossard wakabadilishana.
Na sasa Partey hakufurahishwa na kutoanza mchezo huo pale London Magharibi, katika mechi ambayo ilikuwa mojawapo ya mechi kubwa zaidi za Arsenal msimu huu hadi sasa, na kwamba kambi yake inazidi kuchochewa na kupunguzwa kwake kwa dakika.
Kwa hali ilivyo, Partey yuko tayari kurudisha nafasi yake katika upande wa kiungo mkabaji, lakini vyanzo vimethibitisha kuwa atazingatia chaguzi zake wakati wa Krismasi ikiwa hali haijabadilika.
Arsenal walikuwa wameonesha nia ya kumuuza Partey mapema katika dirisha la usajili la majira ya joto, lakini hatimaye waliamua kubaki na Mghana huyo licha ya klabu za Saudia na Juventus kumtaka.
Washika Bunduki hao bado wana nia ya kumnunua Douglas Luiz wa Aston Villa, baada ya kutuma ofa tatu ambazo hazikufanikiwa mwaka 2022 kwa Mbrazil huyo ambaye alikuwa katika kiwango cha cha juu.
Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Edu pia amekuwa nchini Brazil hivi majuzi akiangalia walengwa wanaoweza kuwasajili huku Andre Trindade wa Fluminense akiwavutia.