Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera ameipongeza TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13), na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Bendera amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio. Pia, amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani humo.

Aidha, Bendera aliwaasa makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha. Amewaahidi wakazi wa Manyara kuwa atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha vizuri mkoa huo.

CECAFA Yatangaza Ratiba Ya Kagame 2015
Makamba: Anayemwaga Fedha Kusaka Urais Hafai