Umoja wa Mataifa (UN), umesema bendera ya Umoja wa Mataifa itapepea nusu Mlingoti katika Makao makuu ya Umoja huo yaliyopo New York Marekani Ijumaa Machi 26, 2021 (siku ya mazishi Kitaifa) kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania.

Hatua hiyo ya UN ni kuungana na Watanzania nan chi wanachama kuomboleza kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha, ofisi ya itifaki imesema ofisi zote za Umoja wa Mataifa duniani zimehimizwa kufanya hivyo pia.

Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena Jiini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya moyo.

Simba SC: Tutampa zawadi Magufuli
Jamal Salami atimuliwa Casablanca