Kuanza vyema kwa kikosi cha Mtibwa Sugar katika ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu wa 2017/18, kumeanza kuwapa hali ya kujiamini baadhi ya wachezaji, kwa kuhisi hakuna atakaeweza kuwazuia kwenye harakati za kusaka taji la ubingwa.

Mmoja wa wachezai walionyesha kujiamini huko ni mlinda mlango wa kutumainiwa kwa sasa huko kwenye mashamba ya miwa Benedictor Tinocco, ambaye alionyesha kiwango kikubwa wakati wa michezo dhidi ya wakongwe Simba na Young Africans mwezi uliopita.

Tinocco amesema kwa sasa wapo vizuri na hana shaka na mwenendo wa kikosi chao, licha ya kuanza kubezwa na baadhi ya wadau wa soka nchini kwa kusema imekua ni kawaida kwa Mtibwa Sugar kuanza kwa kasi na kisha kupotea kwenye njia ya kuusaka ubingwa.

Mlinda mlango huyo ambaye aliwahi kusajiliwa na klabu ya Young Africans amesema, maneno hayo ya wasioitakia mema Mtibwa Sugar yataendelea kukosa nguvu siku hadi siku, na amewataka kuendelea kusubiri na kuona kama wanayoyataka yataweza kutokeza katika mshike mshike wa ligi kuu msimu huu.

Tonocco ametoa tambo za kuamini ubingwa msimu huu una kila sababu ya kuelekea Manungu, huku kikosi cha Mtibwa Sugar kikitarajia kushuka dimbani siku ya Jumamosi dhidi ya Ndanda ya mkoani Mtwara.

Kuelekea katika mchezo huo, kipa huyo amesema kuwa watautumia mchezo huo kuhakikisha wanapata ushindi utakaofanya kuwa tofauti na wanaoshindana nao katika msimamo wa ligi.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kinatarajiwa kuanza safari kesho asubuhi kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Azam FC wao wamekusanya pointi 16 katika michezo 8 na kushika nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya Simba na Young Africans wanaolingana pointi wakitofautiana magoli ya kufunga .

Mkurugenzi Mkuu Acacia ajiuzulu
Wachina 9 wanyang'anywa hati za kusafiria