Beki wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Benedikt Hoewedes, atalazimika kusubiri kwa majuma manne ama zaidi, kurejea tena uwanjani, kufuatia majeraha ya paja yanayomkanili kwa sasa.

Juventus FC wamethibitisha taarifa za beki huypo kutoka nchini Ujerumani kupitia toviti ya klabu hiyo yenye maskani yake mjini Turin.

Hoewedes mwenye umri wa miaka 29, alipatwa na majeraha ya paja mwishoni mwa juma lililopita akiwa katika mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa ligi ya Sirie A dhidi ya Torino.

Kwa matarajio ya muda wa kupona kwa Hoewedes, atakosa michezo ligi dhidi ya Atalanta na Lazio, ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Olympiakos na Sporting Lisbon, na kwa upande wa timu ya taifa, beki huyo atashindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani wakati wa michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Ireland ya kaskazini na Azerbaijan.

Hoewedes, tayari ameshaitumikia Ujerumani katika michezo 44, na alisajiliwa na Juventis FC mwezi uliopita akitokea Schalke 04 kwa mkopo.

Wafanyakazi benki wanyimwa kutumia simu zao, wapangiwa muda maalumu
Sakata la Neymar na Cavani lachukua sura mpya