Meneja wa klabu ya Real Madrid, Rafael Benitez amepangua mipango ya klabu za Man Utd pamoja na Arsenal kwa kueleza wazi hatokua tayari kuwaachia wachezaji wake Gareth Bale pamoja na Karim Benzema kuondoka katika kipindi hiki cha usajili.

Bale mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwaniwa vikali na Man Utd, kwa kuwekewa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinakadiriwa kuvunja rekodi ya usajili duniani, huku mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa  Benzema, mwenye umri wa miaka 27 akihitajika huko kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu yaklabu ya Arsenal.

Man Utd, wameripotiwa kuandaa kiasi cha paund million 100, ili kumpata Bale ambaye anaonekana huenda akafanikisha lengo la kuirejeshea heshima klabu hiyo ya Old Trafford, ambayo imekua ikitapatapa kusaka mafanikio tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson.

Arsenal wao wapo tayari kutoa zaidi ya paund million 30 ili kumpata Benzema.

Kufuatia mvurugano huo wa usajili, Benitez amesema amekua akiendelea vyema na wachezaji hao wawili na haoni sababu ya kukubali kuwaachia kwa sasa, kutokana na mipango yake ya msimu ujao kuwahitaji kwa udi na uvumba.

Amesema inafurahisha kuona wachezaji wake wanahitajika kwenye klabu nyingine kwa kiasi kikubwa cha pesa, na anaamini hatua hiyo inatokana na ujasiri wao wa kupambana vyema uwanjani lakini akaendelea kusisitiza hajashawishika kuwatoa kwa sasa.

Man Utd, wamejikita kuiwania saini ya Bale, kwa lengo la kusaka mbadala wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina, Angel Di Maria ambaye wakati wowote atakamilisha usajili wa kujiunga na klabu bingwa nchini Ufaransa, Paris St German kwa ada ya uhamisho wa paund milioin 44.5.

Arsenel wao wanamuhitaji Benzema kwa lengo la kutaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambayo imekua ikimtegemea sana Olivier Giroud.

Man Utd Wamalizana Na Lyon Ishu Ya Rafael
Nuh Mziwanda Na Shilole Wazungumzia Sauti Ya Nuh ‘Akimtongoza’ Wema Sepetu