Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe imepatiwa shilingi Mil. 400 kwaajili ya ukarabati wa huduma za afya katika Hospitali ya Palangawano inayo hudumia wakazi wengi wa halmashauri hiyo ambayo inatumika kama ya hospitali ya wilaya.
 
Akiongea kuhusu kuhusu fedha hizo Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe Eng. Gerson Lwenge amesema kuwa fedha hizo za Benki ya dunia ambazo wamepata zinatakwenda kurekebisha kituo cha afya cha Palangawano na kujenga wodi na nyumba za watumishi.
 
“Wanging’ombe tumepata kituo kimoja tumeangalia hapa Igwachanya hatuna hata Zahanati ya Serikali wala kituo cha afya hivyo tumeteua kituo cha Palangawano fedha za Benki ya dunia ziende pale zitarekebisha kituo kile cha afya, zitajenga na wodi pamoja na nyumba mbili za watumishi na kuna vifaa vinakuja vya milioni mia tatu kwa hiyo ina maana hata oparesheni za uzazi zitakuwa zinafanyika pale pale. Milioni mia nne zimeshakuja kwenye halmshauri,”amesema Lwenge
 
  • TRA: Hatuhitaji kulumbana na Askofu Kakobe
  • Kisa cha raia wa kijerumani kuuawa kwa kisu Zanzibar
  • TCRA yawalima faini Star TV, Azam TV kuhusu uchaguzi wa madiwani
 
Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo, Ally Kasinge amesema kuwa wilaya yake inamikakati ya kuboresha huduma za afya na halmashauri inatarajia kujenga zahanati kumi na vituo vya afya vinne

Magazeti ya Tanzania leo Januari 3, 2018
Dkt. Kigwangalla, UNDP kuunda kikosi kazi cha uchunguzi