Benki ya Maendeleo ya Wakulima (TADB) imesema kuwa ili kukipatia gawio kiwanda cha kusindika na kuchakata Kahawa ‘TANICA’ ni lazima kuingia makubaliano na vyama vikuu vya ushirika mkoani Kagera vya KCU na KDCU ili kuwezesha kuwa na Malighafi za kuendesha kiwanda hicho.
Hayo yamesemwa na Mkurungenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Japhet Jastine wakati wa makabidhiano baina ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bregadia Jenerali, Marco Gaguti na uongozi wa benki uliofika kwa lengo la kutatua changamoto ya malighafi pamoja na upatikanaji wa mashine za kisasa ndani ya kiwanda hicho.
Amesema kuwa kwa kuvitambua viwanda ambavyo vinafanyakazi ya kuongeza thamani ya mazao na kuweka ubora ambao matumizi makubwa ni wateja wa ndani na nje ya nchi lazima kutumia vyama vya ushirika kupata malighafi ya kutosha.
“Tunatambua kabisa wateja wetu wa Kahawa ni watu wa nje, sisi si watumiaji wakubwa wa Kahawa hivyo ili uweze kupata masoko ya uhakika lazima iwe katika ubora wenye mnyororo wa thamani na malighafi tunapata kwa vyama vyetu vya ushirika,”amesema Jastine
Aidha, amesema kuwa uwepo wa kiwanda hicho hutegemea vyama vya ushirika ambavyo vinakusanya malighafi na kukipelekea kiwanda hicho ili kiweze kuongeza thamani zao na kupatiwa soko.
Kwa upande wake Meneja wa kiwanda hicho, Linus Leopord amesema kuwa kiwanda hicho kinazalisha tani 101 kwa muda wa mwezi baada ya kusindika Kahawa ya unga ambayo ndiyo husambazwa hivi sasa.
Amesema kuwa endapo malighafi ikipatikana kwa wingi uwezekano wa kuzalisha tani 250 kwa mwezi utafikiwa na kupata kipato cha kuendesha kiwanda na shughuli za kiutendaji kupitia wafanya kazi zitafanyika.
-
DataVision International yashinda tuzo ya ‘Brand Leadership’ Afrika Mashariki
-
Video: JPM aikingia kifua Taifa Stars, ‘Kwenye mpira lolote linaweza kutokea’
-
Pierre, Wabunge warejea nchini kimyakimya, ‘Unataka kuilaumu Stars, Senegal wanamishahara mikubwa’
Nao, wafanyakazi wa kiwanda hicho wameonyesha kufurahishwa na ujio wa ugeni huo ambapo wamesema kuwa wameanza kupata matumaini ya kupata mshahara mzuri kulingana na wanavyopata kwasasa.