Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania, kuzifutia leseni benki zote za biashara na za wananchi zitakazoshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli za kibiashara nchini.

Ameyasema hayo mjini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango katika mkutano maalum wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT)

Amesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania ilitoa muda hadi mwisho wa mwezi Desemba 2017 kuwa benki za wananchi ziwe zimeongeza mitaji na kuwa muda hautaongezwa na wala serikali haitatoa mtaji kwa benki hizo.

“Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania, haitasita kuzifutia leseni benki zote za wananchi ambazo zitakuwa hazijatimiza masharti yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi ambao unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja,”amesema Majaliwa

Hata hivyo, maagizo hayo yamekuja siku moja mara baada ya Rais Dkt. John Magufuli kuiagiza Wizara ya fedha na Mipango wakati akifungua tawi la CRDB mjini Dodoma, kuhakikisha Benki Kuu ya Tanzania- BoT inazifuta benki zote zinazoshindwa kujiendesha kibiashara hata kama zinamikiwa na serikali.

 

 

Zitto aipigia chapuo Zanzibar Heroes
Mahakama yaamuru watoto waliotumikishwa walipwe