Mshambuliaji mpya wa klabu ya Liverpool Christian Benteke, amelazimika kuyatoa ya moyoni kumjibu aliyekua meneja wake huko Villa Park yalipo makao makuu ya klabu ya Aston Villa, Tim Sherwood.

Benteke, ameonyesha kuchukizwa na kauli iliyowahi kutolewa na meneja huyo wa kiingereza, wakati akiwa katika mchakato wa kuhamia kwenye klabu ya Liverpool ambayo ilimsajili kwa ada ya uhamisho wa paund million 32.5 majuma matatu yaliyopita.

Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Jamuhuri Ya Kidemikrasia Ya Kongo, amesema Tim Sherwood haikutendea haki klabu ya Liverpool ambayo ina historia kubwa katika ligi ya nchini England pamoja na soka la barani Ulaya.

Tim Sherwood, aliibeza Liverpool kwa kusema haina hadhi ya kuwa na Benteke kutokana na uwezo wa mshambuliaji huyo huku akilinganisha mapigo ya mipira 409 iliyopigwa kutoka pembeni (crosses) na klabu hiyo ya Anfield msimu uliopita kwa kusisitiza yalikua hayakidhi kwa mtu huyo.

Benteke amesema umefika wakati wa kumuhakikishia Tim Sherwood, hakua sahihi kwa maneno hayo ambayo yeye binafsi aliyapokea ndivyo sivyo.

Amesema jukumu lake kubwa ni kucheza soka la uhakika huko Anfeld na kufunga mabao kama ilivyo kawaida yake, ili kuwaziba midomo watu walioubeza usajili wake akiwepo meneja huyo ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Spurs kabla ya kutimuliwa mwaka 2014.

Benteke, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool ambacho kitaanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa nchini Uingereza, mwishoni mwa juma hili kwa kupambana na Stoke City.

Lowassa Adai Akiingia Ikulu Nchi Itatulia ‘Tuli’, Ausuta Uchumi Wa JK
Mwanafunzi Wa ‘PhD’ Aliyeua Watu 12 Asamehewa Hukumu Ya Kifo