Wababe wa soka mjini Madrid, Real Madrid wamethibitisha kuwa mshambuliaji wao kutoka nchini Ufaransa, Karim Benzema anasumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja.

Klabu hiyo imelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya mashabiki kutomuona Benzema  kwenye kikosi cha Real Madrid ambacho kipo nchini Ujerumani kikishiriki michuano ya kombe la Audi.

Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya klabu hiyo nguli nchini Hispania, zimeeleza kwamba siku moja kabla ya kikosi cha The Galacticos hakijaanza safari kuelekea mjini Munich, Benzema alifanyiwa vipimo vilivyobaini kuwa ana matatizo ya misuli ya paja.

Hata hivyo, hatua ya mshambuliaji huyo kutokuwepo kwenye msafara wa kuelekea nchini Ujerumani, iliendelea kuchagiza tetesi za usajili wake kwenye klabu ya Arsenal ambayo inatajwa kumuwania kwa dau la zaidi ya paund million 40.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Benzema kukosa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Real Madrid kuelekea msimu mpya wa ligi huko nchini Hispania, baada ya kuachwa katika safari ya mashariki ya mbali ambapo Real Madrid waliweka kambi ya juma moja nchini China.

Ni Ubabe-Ubabe CCM na Ukawa, Nani Zaidi?
Taarifa Za Seif Sharif Na Profesa Lipumba Kuvurugana Zapata Majibu