Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, Pep Guardiola amesema kikosi kipo kwenye matatizo baada ya Bernardo Silva kuumia na kuongeza idadi ya majeruhi klabuni hapo.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno aliumia na kutolewa kabla ya mapumziko katika mchezo ambao Man City iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Red Star Belgrade juzi Jumanne (Septemba 19) katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Guardiola tayari anawakosa mastaa wake Kevin de Bruyne, John Stones, Mateo Kovacic na Jack Grealish kutokana na kuwa majeruhi.

Baada ya mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Guardiola alisema: “Bila shaka, Bernardo hataweza kucheza mechi zijazo.

Tupo kwenye matatizo, lakini ndivyo ilivyo. Sisemi kwamba tuna majeruhi wengi, lakini ipo hivyo. Ningependa niwe na wachezaji wangu wote, lakini mambo ni lazima yaendelee.”

Bosi Tottenham Hotspur afichua usajili wa Kane
Linah atupwa Jela miaka miwili kwa kukufuru