Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Golden Ratio of Beuty zimemtaja Beyonce kuwa ndiye mwanamke wa pili mwenye mvuto zaidi duniani akifungana na mwanamitindo Bella Hadid ambae ametajwa kuwa namba moja.

Katika tafiti hizo inaelezwa walizingatia zaidi uzuri wa umbo, mdomo wakuvutia, pua, shingo, kidevu, nywele, paji la uso na nyusi.

Ambapo Beyonce amepitwa na Bella Hadid kwa asilimia 1.91 mara baada ya Bella Hadid kuibuka kidedea kuwa na viungo pamoja na umbo lenye mvuto zaidi kulinganisha na wanawake wote duniani.

Katika utafiti huo uliofanywa umebainisha warembo hawa kuwa na mvuto kwa asilimia zifuatavyo.

Upande wa Beyonce yeye alikutwa uzuri kwa asilimia zifuatavyo: paji la uso 92%, nywele zake za Brown 93%, Kope 87%, eneo jicho linapopatikana 94.7%, mdomo 95.7%, shepu ya uso 93%, pua 89%, kidevu 92.2%, upana wa pua 88%.

Alama hizo zinamfanya Beyonce kuwa mwenye uzuri na urembo wa asilimia 92.44% duniani.

Huku Bella Hadid ambaye ameshikilia nafasi ya kwanza ameibuka kidedea kwa kupata pointi zifuatazo.

Uzuri wa umbo la uso wake asilimia 94.5, midomo 94.1%, kidevu 99.7%, paji la uso 97%, pua 93.3%, kope 97.65%, eneo jicho linalopatikana 97.65%.

Alama hizo zinamfanya Bella kuwa mrembo wa kwanza duniani kwa asilimia 94.35.

Aidha, warembo ni wengi duniani ila kwa mujibu wa tafiti na vigezo vilivyozingatiwa na Golden Ratio of Beuty vimewataja wawili hao kuvunja rekodi ya kuwa wanawake wenye mvuto na wzuri zaidi duniani.

 

HESLB yaanika wanafunzi 30,675 waliopata mkopo 2019/2020
Dar yaibuka kinara uandikishaji wapiga kura