Mama mzazi wa mwanamuziki nguli nchini Tanzania, Diamond Platnumz, Sandra Kasim ameachia picha mtandaoni na kuwaacha watu vinywa wazi kwa mshangao baada ya kuibuka madai ni mjamzito na hivyo anatarajia kuongeza mtoto wa tatu.

Akihojiwa na kituo kimoja jijini Dar es Salaam, Sandra alithibitisha kuwa mjamzito na kwamba baba wa mtoto wake nambari tatu ni Rally Jones.

Diamond atapata mdogo wake…basi subirieni mdogo wake wa mwisho,”Sandra alisema.

Baada ya uhusiano wake na Jones kuwa wazi, mama huyo wa watoto wawili alisutwa sana baada ya wengi kudai alikuwa akiiga vitendo vya Zari Hassan na kukimbilia mchumba wa umri mdogo.

Lakini Mama Diamond alijitokeza na kukanusha madai hayo na kusema, Jones si mtoto mdogo na kwamba yeye hajali kuhusu umri katika uhusiano wake wa kimapenzi.

Nimeolewa… Ana udongo gani? Angekua mdogo singeona. Ni mkubwa,” alisema.

Mapema mwaka huu, Jones alizua kimbunga mtandaoni kwa kumwita mama ya msanii huyo ‘mke’ wangu na kufanya watu kuhisi wawili hao walifanya harusi ya siri.

Alichapisha picha akiwa amemshika Sandra mkono na kusema kuwa, uhusiano wao ulikuwa ikiendelea vizuri sana.

Nahisi furaha sana nina mwanamke spesheli kando yangu. Mungu na akupe maisha marefu Inshallah. Happy Birthday mke wangu Mama Dangote. Nakupenda,’‘ aliandika.

Cardi B akabiliwa na kifungo jela kwa kupigana kisa mapenzi
Rais Magufuli na mkewe wamwaga mamilioni feri