Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi wamekubaliana kuongeza matumizi ya fedha za nchi badala ya za kigeni kwenye Biashara kati ya nchi hizi mbili.

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja na Waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao ya faragha, Waziri Mkuu Modi amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza biashara na kupunguza gharama.

Hatua hiyo, itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya dola za Marekani kwenye nchi hizo kwani kwa sasa (kwa takwimu za India 2022/23) thamani ya biashara ya India na Tanzania imefika dola bilioni 6.7 (zaidi ya shilingi trilioni 14) – ongezeko kubwa kutoka dola bilioni 3.2 mwaka 2021/22 (kwq takwimu za Tanzania).

Sterling kumshaiwshi kocha mkuu Engalnd
TPBRC: Ni zamu ya mabondia Wanawake