Serikali nchini, inatarajia kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kufuatilia na kuhakikisha kodi husika za Serikali zinalipwa kwa wakati.

Hatua hiyo itajumuisha matangazo ya biashara ambayo huwekwa na watu maarufu (digital influencers) na biashara za mtandaoni zinazofanyika nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwiguli Nchemba ameyasema hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa pia Serikali imeomba kupunguza Ushuru wa Bidhaa kutoka shilingi 4,386 kwa lita hadi shilingi 2,466.45 kwa lita kwenye vinywaji vikali, vinavyozalishwa nchini.

Aidha, ameomba kusamehe ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini (engine capacity) kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19; 8703.80.10 na 8703.80.90 na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG).

Habari Picha: Uapisho wa Viongozi wateule Ikulu
Kocha Nabi atoa neno la shukurani Young Africans