Kocha Mkuu wa Biashara United Mara, Francis Baraza, amesema mchezo wa mzunguuko watatu dhidi ya Simba itakuwa ngumu kwa sababu wanacheza na timu yenye kibarua kimoja cha kutetea ubingwa wanaoushikilia.

Baraza amesema wataingia uwanjani kwa  kuwaheshimu, lakini wakiwa na lengo la kutafuta alama muhimu katika mchezo huo wa ambao utapigwa majira ya saa moja usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Septemba 20.

Kocha huyo kutoka nchini Kenya amesema licha ya kupata ushindi katika michezo yao miwili iliyopita, hawatabweteka na ataendelea kupanga mbinu zaidi za ushindi dhidi ya vigogo hao wa soka la bongo.

Ameeleza maandalizi ya mchezo huo anayafanya tofauti na jinsi alivyocheza michezo yao miwili iliyopita dhidi ya Gwambina na Mwadui FC, kwa sababu ya aina ya wachezaji wanaotarajia kukutana nao.

“Mchezo huo ni ngumu, hatuwaogopi ila ninawaheshimu. Watu wanatakiwa watambue tunaenda kucheza na mabingwa, lazima uwape heshima yao, ukizingatia ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri ambao wanaweza kumpa kocha matokeo wakati wowote wanapoamua kucheza,” Amesema Baraza.

Amesema bado anaendelea kukijenga kikosi chake na ameitumia michezo miwili iliyopita kama sehemu ya kuimarisha wachezaji wake kuelekea mchezo huo dhidi ya Simba.

Michezo mingine ya mzunguuko watatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa mwishoni mwa juma hili.

Kenya yasalimu amri watanzania kukaa karantini
JPM aagiza mwalimu mkuu wa shule iliyoungua atolewe mahabusu