Biashara United Mara FC imekata rasmi tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa mzunguuko wa 33 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Biashara United Mara FC itashiriki michuano ya kimataifa kwa nara kwanza kwenye historia ya klabu hiyo kutoka mjini Musoma Mkoani Mara.

Biashara United ilikua inahitaji alama moja tu, kabla ya mchezo wa leo Alhamisi (Julai 15) uliounguruma Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa, Uwanja wa Nelson Mandela.

Matokeo ya sare yanaifanya Biashara United kufikisha alama 50 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote kati ya zile zilizo chini yao.

Timu nyingine itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao ni Azam FC inayokamata nafasi ya tatu.

Simba SC ambao ni Mabingwa mara nne wa Tanzania Bara na Young Africans watashiriki Michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

PICHA: Azam FC yaipongeza Simba SC
Rais Samia kuzungumza na vyombo vya habari Burundi