Mbeya, bibi harusi mtarajiwa, aliyefahaimika kwa jina la Diana amepoteza maisha akiwa na ndugu zake watatu katika ajali ya gari iliyotokea pindi wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya sherehe ya kumuaga binti huyo maarufu kama ‘send off’ iliyotakiwa kufanyika Juni 29, 2019.

Katika ajali hiyo wengine waliofariki ni pamoja na Faraja Mwandunga, James Mwandunga na Jacton mwenye umri wa miaka 2 ambaye ni mtoto wa Faraja Mwandunga na majeruhi katika ajali hiyo ni Ibrahimu Mwandunga na Nico Mwandunga ambao walikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya.

”Mimi na ndugu zangu wengine tulitangulia kuja Dar es salaam ila yeye na wadogo zangu ambao wamepata ajali hiyo walibaki”. amesema kaka mkubwa wa bibi harusi mtarajiwa.

Ajali hiyo imetokea kutokana na uzembe uliosababisha na dereva wa gari dogo wakati anataka kulipita gari kubwa aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa limeharibika barabarani kwani gari hilo dogo liligonga gari kubwa na kukosa mwelekeo na kupindukia mtaroni.

Mkuu wa usalama barabarani wa Mkoa wa Mbeya, RTO, Jumanne Mkwama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa hadi sasa jeshi la polisi linamtafuta dereva wa gari kubwa kwani mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo alikimbia.

Bwana harusi mtarajiwa, Elisante Edward alizipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa sana akiwa njiani kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufunga harusi hiyo na Diana na mara baada ya kupokea taarifa hiyo alilazimika kushuka Chimala kuendelea na taratibu nyingine za mazishi.

Aidha, waliofariki ni watoto wa familia moja waliozaliwa kwa kufuatana ambapo Faraja alikuwa mkubwa akifuatiwa na James kisha Diana ambae alikuwa mdogo wao.

 

 

 

 

 

Jeshi la Marekani limekiri ndege yake kutunguliwa na Iran
LIVE: Harambee ya kuichangia timu ya taifa 'TAIFA STARS'

Comments

comments