Sarah Obama, Bibi wa Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga Kisumu nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea masikitiko yake na kutuma salamu za rambirambi kwa Familia ya Obama kufuatia kifo hicho ambapo amesema, “hili ni pigo kwa Taifa letu, tumempoteza Mwanamke shupavu, aliyeiunganisha Familia ya Obama.”

Vilevile Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Ida Odinga wametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Obama kufuatia kifo cha Bibi Sarah Obama ambaye amefariki leo asubuhi.

“Tumempoteza Mwanamke mpambanaji ambaye aliishi mbele ya muda, aliweza kuendesha Familia yeye mwenyewe baada ya Mumewe kuondoka, amekuwa mfano bora wa Wanawake majasiri akiwa na uwezo wa kipekee wa kukabiliana na changamoto na alikuwa chachu kwa mjukuu wake Barack Obama kukuza Elimu kwa Watoto wa Kike,” imeeleza taarifa sehemu ya salamu za rambirambi kutoka kwa Familia ya Odinga.

Bibi Sarah Obama alimtetea mjukuu wake wakati wa uchaguzi wa Marekani iliposemekana ni Muislamu na hakuzaliwa Marekani.

Sarah ambaye ni mke wa tatu wa Hussein Obama amefariki akiwa na umri wa miaka 99 na atazikwa leo, Machi 29, 2021 kwa taratibu za dini huko Kogelo.

Mwenyekiti UVCCM: Tuombe radhi, tuanze upya, tumsaidie Rais Samia
Manara: Aishi ndio MVP wangu msimu huu