Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameondoa kikwazo kilichokua kimewekwa na Utawala wa Donald Trump kwa Watanzania kutoruhusiwa kuomba Viza ya Bahati Nasibu (Diversity VISA-DV) ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutangazwa kwa vikwazo hivyo.

Uamuzi huu ni miongoni mwa maamuzi aliyoyafanya Biden ndani ya siku mbili toka kuapishwa kwake.

Januari 30, 2020 serikali ya Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa.

Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa utawala uliopita wa Trump,  nchi hizo ziliwekewa marufuku hiyo kwa kushindwa kufikia “kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa”.

“Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbalimbali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka,” aliyekuwa Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf aliwaambia wanahabari baada ya kutangazwa kwa vikwazo.

Seneti kumuidhinisha Waziri wa kwanza Mweusi wa Ulinzi
Balozi Ibuge akutana, kufanya Mazungumzo na AG Zanzibar

Comments

comments