Rais wa Marekani, Joe Biden ametishia kuirejeshea Myanmar vikwazo baada ya Jeshi la nchi hiyo kuchukua madaraka, huku likikataa kukubali matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Novemba 2020.

Biden amesema nguvu haipaswi kupindua matakwa ya wananchi au kujaribu kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Kidemokrasia akisisitiza kuwa Marekani itasimamia Demokrasia pale inapohatarishwa.

Chama cha Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, ambaye anashikiliwa pamoja na Maafisa wengine kinashutumiwa kwa udanganyifu kufuatia ushindi wake katika Uchaguzi.

Jeshi la Myanmar tayari limebadili Mawaziri na Manaibu 11 wakiwemo wa Fedha, Afya, pamoja na Mambo ya Nje na Ndani.

Umoja wa Mataifa (UN), Uingereza, Umoja wa Ulaya (EU) pia wamekemea kinachoendelea, na kuna hofu ya  kutokea maandamano na vurugu.

Simba SC kuifuata Dodoma Jiji, kutinga bungeni
Bulaya ataja anachokitaka Bungeni