Mgombea urais Nchini Marekani, kupitia chama cha Democratic Joe Biden, ameshinda uchaguzi wa Urais nchini humo dhidi ya mpinzani wake Donald Trump mara baada ya kushinda katika majimbo yaliyochukuliwa na Republican mwaka 2016.

Kwa mujibu wa vituo vya televisheni vya CNN, NBC News, CBC News, vimetangaza kuwa mchuano huo umeishia kwa Biden kuibuka kidedea baada ya kukadiria ushindi katika jimbo ambalo lilitarajiwa kuamua mshindi la Pennsylvania.

Ushindi wa Biden umemaliza utawala wa Rais Trump uliotingisha siasa, na kuiacha Marekani ikiwa imegawanyika zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Vituo hivyo vya Television vilimpa ushindi Biden muda mfupi kabla ya saa 5:30, asubuhi baada ya kura za jimbo la Pennsylvania kuwa na tofauti kubwa isiyoweza kufikika na hivyo kuwa juu katika majimbo yanayoamua mshindi wa uchaguzi wa urais.

Biden, mwenye umri wa miaka 77, ni mgombea mwenye umri mkubwa kuwahi kuchaguliwa kuingia ikulu ya Mrekani, huku Trump akiwa na miaka 74 ametoa malalamiko yasiyo na ushahidi dhidi ya wizi mkubwa wa kura huku timu yake ya kampeni ikiwa imefungua kesi katika majimbo kadhaa.

Bunge la 12 kuanza rasmi Novemba 10
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 8, 2020

Comments

comments