Kufuatia Uchaguzi wa Urais nchini Marekani unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Marekani, Kamala Harris ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Mgombea Urais kupitia chama cha Democratics Joe Biden, amekubali kuwa mgombea mwenza ili kumuondoa Rais Trump.

Hayo yamejiri katika mkutano wa chama hicho mara baada ya Harris kushindwa katika kura za maoni zilizompendekeza Biden kuwa mgombea kupitia chama hicho.

Kamala Harris mwenye umri wa miaka 55 na Biden 77,  wamejipanga kumpindua Rais Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Aliyemshinda Gwajima kura za maoni Kawe afunguka
Orodha ya waliopitishwa kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM, Gwajima, FA wapeta