Rais mteule wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kumchagua mwanasheria mkuu wa jimbo la California Xavier Becerra kuwa Waziri wa Afya.
Uteuzi wa Becerra mwenye umri wa miaka 62, ambaye pia alikuwa anatajwa kuwa chaguo la Mwanasheria Mkuu, unakuja wakati ambapo Biden anakabaliwa na shinikizo la kuchagua watu wa matabaka mbalimbali katika baraza lake la Mawaziri.
Iwapo atathibitishwa na seneti, atakuwa na jukumu muhimu katika baraza la mawaziri la Biden, kwa kuwa tayari rais huyo mteule ameonyesha kuyapa kipaumbele mapambano dhidi ya janga la COVD-19.
Akiwa mwanasheria mkuu wa California, Becerra aliongoza juhudi za kisheria za kulinda mpango wa afya wa Obama maarufu Obama Care, uliotoa fursa pana ya huduma za afya na ulinzi.
Mwaka 2017 Becerra aliapa kuwa Mwanasheria mkuu wa kwanza wa asili ya Latino katika jimbo hilo la California na amekuwa akihusishwa sana na nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Marekani