Rais mteule wa Marekani, Joe Biden atatia saini maagizo ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais januari 20, 20201 ili kushughulikia janga la virusi vya corona, uchumi wa nchi hiyo unaodorora, mabadiliko ya hali ya hewa na ubaguzi wa rangi. 

Kwa mujibu wa mkuu wa utumishi anayetarajiwa Ron Klain amesema kuwa mizozo hiyo inatakiwa kushughulikiwa kwa haraka ili nchi hiyo irudi katika hali yake ya kawaida.

Aidha ameongeza kuwa Biden,atatia saini ya takriban maagizo 12 ya rais baada ya kuapishwa siku ya Jumatano. 

Klain aliongeza kuwa katika siku zake 10 za kwanza ofisini, Biden atachukua hatua madhubuti kushughulikia mizozo hiyo minne, kuzuia madhara mengine ya haraka na yasiyoweza kurekebishwa, na kurudisha nafasi ya Marekani ulimwenguni.

Museveni awaonya watakaoanzisha ghasia
Watanzania tuongeze juhudi katika hili