Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa nchi tatu za Baltic katika mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami ya NATO katika hatua ya kuzihakikishia tena nchi hizo uungaji mkono wa Marekani,

Kwa mujibu wa Idhaa ya kiswahili ya Ujerumani (DW), taarifa imesema kuwa Rais Biden hajakutana siku ya Jumatano na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini Geneva.

Ikulu ya Marekani imeeleza kwamba Biden amekutana leo na waziri mkuu Kaja Kallas wa Estonia,rais Egils Levits wa Latvia na rais Gitanas Nausenda wa Lithuania na kuwahakikishia kwamba Marekani inawaunga mkono kwa dhati katika suala la usalama wao.

Viongozi hao wamezungumzia hatua zaidi za kuimarisha ushirikiano wa kisiasa,kijeshi na Kiuchumi ikiwemo kufanya kazi pamoja kupitia jumuiya ya NATO kushughulikia changamoto zinazosababishwa na Urusi na China.

RC Kunenge aagiza uchuguzi kwa watumishi Mkoa wa Pwani
Wahadhiri wenye miaka 60 waendelee kufundisha