Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Urusi Vladmir Putin wamekutana leo kwa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana tangu Biden aingie madarakani.

Viongozi hao wawili wamesema wanatumai mazungumzo yao yanayofanyika jijini Geneva, yataimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili, ingawa wanatofautiana kwa kila kitu kuanzia udhibiti wa silaha na udukuzi wa mitandaoni hadi uingialiaji uchaguzi na mzozo wa Ukraine.

Aidha mahusiano kati ya Washington na Moscow yameharibika kwa miaka mingi, hasa baada ya Urusi kunyakua eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014.

Uingiliaji wake katika vita ya Syria mwaka 2015 na madai ya Marekani – yaliyokanushwa na Urusi – ya kuingilia katika uchaguzi wa 2016 ambao ulimuingiza Donald Trump katika Ikulu ya White House.

Mwezi Machi, Biden alimuita Putin muuaji, hatua iliyoifanya Urusi kumuita nyumbani Balozi wake wa Washington kwa mazungumzo huku Marekani nayo ikamuita Balozi wake mwezi Aprili.

Rais Samia ateua Wenyeviti wa Bodi, Anne Makinda astaafu
Tanzania, Marekani kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza