Rais wa Marekani, Joe Biden ameliambia bunge la Congress kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin alikosea kimtazamo kuhusu namna nchi za Magharibi zingejibu mapigo wakati alipoivamia Ukraine.

Katika hotuba yake hiyo, Biden ameapa kuwa “Uamuzi usioyumba kwamba daima uhuru utashinda dhidi ya udhalimu.”

Hotuba hiyo inakuja wakati Wamarekani wanaonekana kuchoshwa na janga linalowafanya kukabiliana na mfumuko wa bei za mafuta na vyakula baada ya vita hiyo ya Urusi na Ukraine.

Rais huyo wa Marekani kupitia chama cha Democratic aliwaambia wabunge Jumanne usiku kuwa Putin alikataa juhudi za mara kwa mara katika diplomasia na vita vyake vilipangwa na havina sababu.

“Alidhani nchi za Magharibi na NATO zisingechukua hatua. Na, alidhani angeweza kutugawanya hapa nyumbani. Putin alikosea. Tulikuwa tayari.”

Biden alitangaza kuwa Marekani itapiga marufuku ndege za Urusi katika anga yake, kama zilivyofanya mamlaka za Canada na Ulaya.

Dkt. Kijaji ataja sababu za kupandishwa bendera ya Tanzania Burj Khalifa
GGM yapongezwa na Bunge kwa kusimamia masuala ya UKIMWI