Mivutano na vita vya maneno vinazidi kushika kasi ndani ya klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona kati ya makamu wa Rais aliyejiuzu, Emil Rousaud, na Rais Josep Maria Bartomeu.

Rousaud amesema yuko tayari kuingia kwenye vita vya kisheria na Rais Bartomeu, kutokana klabu hiyo kunuka rushwa ya wazi, na kwamba jitihada za klabu kukabiliana na malalamiko yake ni harakati za kumchafua.

Hivi karibuni, Rousaud na wenzake watano walijiuzulu nafasi zao kupinga namna klabu hiyo inavyoendeshwa na utawala wa Rais Bartomeu.

Miongoni mwa mambo waliyoyalamikia ni kashfa ya mitandao ya kijamii iliyopewa jina la ‘BarcaGate’  ambapo Rais Bartomeu anatuhumiwa kuajiri kampuni ya kumpamba kupitia mitandao ya kijamii, katika kipindi hiki cha mwaka wake wa mwisho kuelekea uchaguzi mkuu.

Kampuni inadaiwa kufanya kazi ya kuwachafua watu wote wanaompinga Bartomeu na kumsafisha yeye, ili kumsafishia njia ya kuwania tena kiti cha urais, klabuni hapo.

Simba SC yamkalia kooni Mwakalebela
Ajali yaua 18 na kujeruhi 15 Mkuranga