Mwanamke mwenye umri wa miaka 70, huko nchini Uganda aliyetambulika kwa jina la Verena, ambaye amekataliwa kimapenzi kwa umri wote wa Maisha yake amejitokeza hadharani na kusema hajakata tamaa na ana matumaini atakutana na mwanamume wake.

Verena ambaye amebaki kuwa bikira kwa miaka 70, anadai kuwa maumbile yake ya kimo kifupi ndio sababu yake kukosa mwanaume akieleza kuwa hana ujasiri wa kukaribia au kuzungumza na wanaume.

Akizungumza na mtandao wa AfriMax, Verena, ambaye ni bikira, alijielezea kwamba ni mtu aliyejawa upendo siku zote na hajawahi bahatika kukutana na mwanamume ampendaye.

“Mimi bado ni bikira. Sijawahi kuolewa, sijawahi kulala na mwanaume na sijui inakuwaje, Bado nina matumaini ya kupata mpenzi na ninaishi maisha ya uchungu kwa sababu huwa naumwa kila mara. Ninakosa pesa za matibabu…” Alisema.

Verena amesema anatumai siku moja atakutana na mwanaume atakayempenda na kuolewa, akiongeza kwamba siku zote alikuwa akitamani kuingia katika ndoa baada ya kufikisha miaka 20, lakini anahofia kwamba anaweza kufa kabla ya kukutana na mpenziwe.

Ahmed Ally: Simba SC hatujapiga hatua kwenda nyuma
Uwanja wa CCM Kirumba kutumika michezo ya Kimataifa