Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Alvera Uwitonze mwenye umri wa miaka 56 anayeishi na ulemavu uliomfanya ashindwe kutembea kawaida anatafuta mume wa kuishi naye kwasababu yuko mpweke, amesema alikuwa na wachumba hapo awali lakini aliogopa kuchumbiwa kwa kuhofia mwanaume angemdhulumu na kumpa ujauzito kisha amkimbie

ALvera amefunguka kuhusu changamoto za kuzeeka bila kuwa na mume ambapo amesema kuwa hajawahi kuwa katika uhusiano wa mapenzi na mwanamume yeyote hapo awali na sasa anatafuta mtu wa kumuoa.

Katika mahojiano na Afrimax English, amesema anajuta kutowapa wanaume nafasi ya kuwa naye walipomkaribia akiwa msichana mdogo.

“Walikuwa wakija hapa na kuniuliza wanioe nikawakatalia wote, niliogopa atakuja mwanaume kunipa ujauzito wakaniacha mimi na mtoto na kuendea mtu mwingine,” alisema.

Alifichua kwamba alipata mwanamume ambaye alikubali kumuoa lakini kwa masharti kwamba amlipe KSh 22,000.

“Ninaishi ndani kabisa kijijini na hakuna njia ya kupata pesa za aina hiyo. Lakini nikipata, bado nitampa kwa sababu niko mpweke na pia nataka kuwa na familia yangu,” alisema.

Alvera, aliyezaliwa bila hali yake ya sasa, alisema wazazi wake walimpeleka kwa mganga badala ya hospitali alipougua. Kwa sasa anaishi pekee yake, akilima shamba lake, anajipikia na ana redio ya zamani ambayo inamsaidia kutoa upweke.

Amesema kuwa , wanaume wengi wanasema kuwa muda wa kumuoa umepita na wanapendelea wanawake wachanga na ambao hawana ulemavu.

Katika taarifa sawia na hiyo, mwanamke mwingine, 70, hivi majuzi aliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kusema kwamba anatafuta mwanamume wa miaka 21 awe mpenzi wake.

Bibi huyo alisema hakuwahi kuwa na mwanamume hapo awali kwa sababu aliogopa kuvunjwa moyo lakini sasa yuko tayari kupenda tena. Ingawa ni mlemavu, alisema hilo halitamzuia kuwa na mwanamume.

Chama awapongeza wachezaji Simba SC
Klopp: Tutapambana hadi mwisho 2021/22