Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili – MOI, imeanzisha huduma mpya ya upasuaji, kufufua na kuziimarisha kwa kufanywa na Watalaamu Mabingwa wa hapa nchini baada ya Serikali kutoa fedha zaidi ya TZS Bil 4.5 kwa ajili ya vifaa.
Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Agosti 3, 2023 jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Prof. Abel Makubi, amesema Huduma hizo ni kama kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia tundu la pua na Wagonjwa 31 wameshafanyiwa upasuaji.
“Na Gharama za upasuaji huu hapa nchini ni Tsh milioni 8 – 16 na nje ya nchi ni zaidi ya Tsh milioni 40, na niwagonjwa wachache sana sahivi ndio wanaenda kutibiwa nje lakini asilimia 99 tunawatibu wenyewe Nchini kwetu”, amesema Makubi.
Hata hivyo, amesema huduma nyingine ni pamoja na matibabu ya maumivu sugu ya mgongo bila ya upasuaji na kwamba toka kuanza kwake Mei 2023 tayari wagonjwa 97 wamepata huduma hiyo na Gharama za upasuaji nchini ni Shilingi milioni moja na nje ya nchi ni zaidi ya milioni 9.
Aidha, Makubi ameongezea kuwa kufufuliwa kwa huduma za Upasuaji Marudio ya vipandakizi kumefanya wagonjwa 57 kwa kurekebisha nyonga na magoti kwa wale ambao walifanyiwa upasuaji kati ya miaka 15-19 iliyopita.
Amesema, “huduma hizi mpya, zimeiwezesha taasisi kupunguza kero za ucheleweshaji wa matibabu na hata wagonjwa wengine kupata madhara ya kudumu lakini pia zimepunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi kwa sasa kwa magonjwa ya Ubongo na mishipa ya fahamu ni asilimia 96 tunafanya hapa na Upasuaji wa mifupa asilimia 98 tunafanya hapa.”