Kwa siku za hivi karibuni barani Ulaya wachezaji wamekuwa wakinunuliwa kwa pesa nyingi pengine kwa thamani ambayo hailingani na viwango vyao uwanjani.

Neymar, Mbappe na Ousmane Dembele wamenunuliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa lakini kuna wachezaji wengine kutoka katika ligi ya Uingereza amabo kwa sasa dhamani yao inaweza kuvunja rekodi. Tazama orodha hii ya wachezaji 5 katka lig ya Epl ambao wana thamani ya juu.

1.Harry Kane. Thamani ya Kane inatajwa kukaribia thamani ya Neymar kwa sasa na Tottenham wanataka zaidi ya Pauni milioni 170 kama unamtaka Kane, tayari Florentino Perez amekanusha kumhitaji Kane lakini ni wazi kwa umri wa Benzema na Ronald lazima Perez atahitaji mtu wakufunga mabao Kane.

2.Phelippe Coutinho. Liverpool walikataa kiasi cha Pauni milioni 118 kutoka kwa Barcelona ikiwa na maana kuwa walitaka pesa kubwa zaidi ambapo Barca wanasema Liverpool walihitaji £200m na hii inamaanisha kwa sasa ni lazima uwe na kuanzia £118m ukimhitaji.

3.Kevin De Bruyne. Wakati Chelsea wakimuuza alionekana mchezaji wa kawaida tu lakini tangu City wamchukue kutoka Wolfburg anaonekana kati ya viungo bora kwa sasa duniani na sasa mchezaji huyo anaweza kufika thamani ya Paunni milioni 110.

4.Dele Alli. Umri mdogo wa Ali, kiwango kikubwa akiwa amefunga mabao 31 toka aanze Epl itakupasa uwe na Pauni milioni 100 kumpata.

5.Eden Hazard. Katika mchezo wa jana dhidi Fc Bournamouth Hazard alifunga bao pekee lililoipa ushindi Chelsea na kiwango chake kinaonekana kuzidi kuimarika baada ya majeraha msimu uliopita, Real wanamtaka na Hazard na Chelsea wako tayari kufikiria ada ya Pauni milioni 100.

Rais wa Iran ashikilia msimamo wake juu ya utengenezaji wa silaha
Tanesco waweka kambi Mbezi