Meneja wa klabu ya West Ham United, Slavan Bilic ameendelea kulia na chama cha soka nchini England FA, kufuatia adhabu ya kadi nyekundu iliyomuangukia mlinda mlango wake Adrián San Miguel del Castillo mwishoni mwa juma lililopita.

Adrian, aliangukiwa na adhabu hiyo kufuatia makossa aliyoyafanya ya kumshika jezi mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, James Vardy wakati alipokua anakwenda kulisabahi lango la The Hammers ambalo lilikubali kuchabangwa mabao mawili kwa moja.

Bilic, ameendelea kulia na FA, kutokana na kuamini mlinda mlango huyo hakustahili adhabu kubwa kama hiyo, kwa madai hakufanya lolote baya kwa kuzingatia kanuni za soka.

Meneja huyo kutoka nchini Croatia amesema muamuzi hakumtendea haki Adrian na wakati mwingine aliamini huenda alikua na kisa nae.

Bilic, amelalamika juu ya suala hilo, kutokana na mipango yake ya kumtumia Adrian katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili kufeli, ambapo adhabu hiyo ya kadi nyekundu itamuweka nje mlinda mlango huyo kutoka nchini Hispania.

West Ham Utd pia itamkosa mshambuliaji wake kutoka nchini Argentina, Mauro Zarate mwishoni juma hili kufutia majeraha nyama za paja yanayomkabili kwa sasa.

Wagonga nyundo wa jijini London, watakua na mpambano dhidi ya klabu iliyopanda daraja msimu huu Bournemouth ambayo itakua nyumbani Dean Court.

Madrid Yajihami Kwa De Gea Wa Man Utd
Coastal Union, Toto African Na Stand Utd Mashakani