Fedha za Bilionea Dkt. Louis Shika zilizokuwa nje ya nchi zimewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili ya kuhakikiwa.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari Jijini Dar es salaam, Dkt. Shika amesema kuwa kiasi cha pesa kilicho wasili ni dola milioni sitini na vipande vya dhahabu akisema kuwa hii ni awamu ya kwanza.

Amesema kuwa baada ya kupata fedha kukamilisha taratibu zilizobaki ataenda kutimiza ahadi yake ya kununua nyumba za Lugumi ili aweze kutimiza ndoto zake za kufungua kampuni.

Aidha, Dkt. Shika amesema kuwa kwasasa ana mpango wa kuzalisha ajira elfu ishirini kwa Watanzania kupitia viwanda 30 ambavyo amepanga kufungua nchi nzima.

“Hela ambazo nilitamka ziko nje ya nchi sasa kiasi kidogo kimeshatua hapa Dar es salaam, hivyo zimepelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili ya kukaguliwa,”amesema Dkt. Shika

Hata hivyo, Dkt. Shika alijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana mara baada ya kushindwa kununua nyumba za mfanyabiashara maarufu nchini Lugumi, kitu ambacho kilimsababishishia kuwekwa rumande kwa tuhuma za kuvuruga mnada.

 

Video: Iliwauma sana ACT- Wazalendo baada ya kuwaaga- Prof. Kitila
Hofu yatanda vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume vyakithiri