Mfanyabiashara na mmoja wa Matajiri Duniani, Jack Ma, anadaiwa kutoonekana hadharani kwa zaidi ya miezi miwili tangu alipoikosoa serikali ya Rais Xi Jinping na Chama cha Central Communist Party (CCP).
Jack Ma aliwashtumu Maafisa wa fedha na Benki za Serikali akiwafananisha na ‘klabu ya watu wazee’ na kushinikiza mabadiliko.
Inadaiwa, matamshi yake yalipelekea Serikali hiyo kufunga shughuli zake za kibiashara nchini humo.
Taharuki ya kutokuonekana kwake imekuwa kubwa baada ya Ma kutohudhuria onesho lake la ‘Africa’s Business Heroes’ Novemba 2020 akiwa kama Jaji ambapo aliwakilishwa na mmoja wa Wakurugezi wa Alibaba Group.