Bilionea Nick Candy amethibitisha kuwa na nia ya kutaka kuinunua Klabu ya Chelsea iliyowekwa sokoni na mmiliki wake, Bilionea wa Kirusi, Roman Abramovic.

Bilionea Candy kutoka nchini Uingereza na shabiki mkubwa wa Chelsea, ametangaza dau la Pauni bilioni 2.5 pamoja na nyongeza ya Pauni bilioni 1.5 kwa ajili ya matengenezo ya Uwanja wa Stamford Bridge, kitu ambacho matajiri wengine waliojitokeza wameshindwa kukifanya.

Candy mwenye umri wa miaka 49, alianza kuishabikia timu hiyo akiwa na umri wa miaka minne huku kila msimu akiwa na tiketi za msimu mzima za kutazama michezo ya Chelsea.

Msemaji wa Candy amesema: “Nick Candy kwa sasa anaangalia baadhi ya masuala kwa ajili ya kuinunua Chelsea.
Ofa yoyote lazima tutaungana na kampuni nyingine na tupo makini na nia ya kuungana na wenzetu wa kimataifa.” amesema Msemaji wa Bilione huyo

Ikumbukwe kuwa Roman Abramovic alisema tarehe ya mwisho ya kupokea ofa kwa ajili ya kuiuza Chelsea ni Machi 15, mwaka huu.

Young Africans Vs KMC FC wasogezwa mbele
DP Ruto: nitapinga ufisadi nikiwa Rais