Eva Godwin – Dodoma.

Kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Shilingi Bilioni 10.99 ziligharamia ufadhili wa miradi 132 ya kuboresha miundombinu ya elimu, katika shule 151 Nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Agosti 10, 2023 Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania – TEA, Bahati Geuzye amesema miradi hiyo ilijumuisha ujenzi wa madarasa 114, katika Shule 38.

Amesema, “katika madarasa hayo 114 shule za msingi ni 36 na sekondary ni mbili, maabara kumi za Sayansi katika Shule tano za Sekondari, pia matundu ya vyoo 888 katika shule 37 za Msingi zikiwa ni 29 na Sekondari nane.”

Hata hivyo, Geuzye amesema TEA ilipokea michango na kutekelezwa kwa miradi ya pamoja na mashirika ya Umma na yasiyo ya Kiserikali yenye thamani ya Milioni 404 toka Taasisi ya SAMAKIBA, TANAPA, BRAC, Taasisi ya Flaviana Matata, CAMARA education Tanzania, Kampuni za Sayari safi na Dash Industries Ltd.

Aidha, ameongezea kuwa kwa mwaka 2023/2024 Mamlaka hiyo imepanga kutumia kiasi cha Bilioni 8 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini kitakachotumika kufadhili miradi 82 katika shule 81 zikiwemo shule 48 za msingi na 33 za sekondari katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.

Kukamilika kwa miradi hiyo, kutanufaisha jumla ya wanafunzi 39,484 na Walimu 169 wa Shule za Msingi na Sekondari.

Mkataba uwekezaji wa Bandari ni halali - Mahakama
Kocha Ferrer aikacha Amavubi