Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.
Halmashauri ya Bukoba Vijijini Mkoani Kagera imepokea kiasi cha Bilioni mbili na Milioni 500 za kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 zitakazotumika katika shughuli mbalimbali na Maendeleo ikiwemo Afya, Elimu na Kilimo.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashari ya Bukoba Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Murshid Ngeze amesema fedha hizo zimepokelewa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambayo imeanza Julai 7 hadi Oktoba 30.
Kwa upande wao Baadhi ya Madiwani wa Halmashari hiyo akiwemo Jasson Rwankomezi wa Kata ya Kaibanja, Privatus Mwoleka Diwani Kata ya Bujugo, Sadoth Ijunga Diwani Kata ya Mikoni wamemshukuru Rais Samia kwa juhudi mbalimbali za kuhakikisha Taifa.
Mwenyekiti huyo wa Halmashari ya Bukoba Vijijini anarejea katika nafasi yake baada ya kuwa nje ya ofisi kwa kipindi kirefu kufuatia ajali aliyoipata Oktoba 2022 hali iliyopelekea kuwa majeruhi na baadaye kukatwa mguu wake wa kushoto, ambapo amewashukuru wale wote waliokuwa wakimuombea hadi kupona kwake.