Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ifikapo mwaka 2024 Mkoa wa Singida hautashuka asilimiq 97 ya upatikanaji wa umeme.
Rais Samia ameyasema hayo katika maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Mkoa wa Singida, yaliyofanyika katika Viwanja vya Bombadia Oktoba16, 2023 mkoani humo.
Amesema, “kwa upande wa Umeme, Naibu Waziri wa Nishati amesema hapa ikifika Desemba mwaka ujao, kama sio asilimia 100, hatutashuka asilimia 97 ya upatikanaji wa umeme ndani ya Singida.”
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema Serikali imetoa shilingi Bilioni 72 kwa ajili ya kuvipatia vijiji vyote 171 ambavyo vilikuwa havijapatiwa umeme ambapo mpaka sasa Vijiji 50 vilivyobakia wakandarasi wako site wanaendelea na kazi.