Mmiliki wa kampuni ya Tesla ya uzalishaji wa magari ya umeme Elon Musk, amempiku mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates na kuingia nafasi ya pili kwenye orodha ya matajiri wakubwa zaidi ulimwenguni.
Kwa mujibu wa takwimu za mabilionea za Bloomberg, kampuni ya hiyo ya Tesla inayomilikiwa na Musk, imepanda kiwango cha hisa kwa asilimia 6.5 na kufikia Dola Bilioni 127 na milioni 900 baada ya ongezeko la Dola Bilioni 7 na Milioni 200.
Musk mwenye umri wa miaka 49, ameweza kuongeza kipato chake kwa Dola Bilioni 100 na milioni 300 tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Kipato cha mwanzilishi wa kampuni ya teknolojia ya Microsoft kutoka Marekani Bill Gates, kimefikia Dola Bilioni 127 na Milioni 700.
Mmiliki wa kampuni ya Amazon kutoka Marekani Jeff Bezos, ameendelea kuishikilia nafasi yake ya kwanza kama tajiri mkubwa zaidi duniani kwa kipato cha Dola Bilioni 182.
Takwimu za mabilionea za Bloomberg huchapishwa orodha ya matajiri wakubwa zaidi kwa umma kwa kuzingatia milki zao, mapato ya hisa na rasilimali zao zenye thamani ya juu.