Hatimaye Kitendawili cha Michuano ya CAF Super League kimeteguliwa mjini Arusha-Tanzania, kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ Patrice Motsepe kutoa ufafanuzi wa kina.
Rais Motsepe amesema michuano hiyo ambayo itachezwa kwa mara ya kwanza Barani Afrika itashirikisha klabu 24, ambazo zitanufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na Bajeti iliyotengwa na CAF.
Amesema Bingwa wa Michuano hiyo atavuna kasi kikubwa cha pesa 9Dola milioni 100 za Marekani)
Akiwa katika Mkutano Mkuu wa CAF mjini Arusha leo Jumatano (Agosti 10) kiongozi huyo amesema: “Ukiacha viwanja tatizo kubwa kwa mpira wa bara la Afrika ni fedha”
“Nimshukuru kaka yangu Gianni Infantino kwa kutupatia wazo hili ambapo kupitia mashindano haya mapya ya CAF SUPER LEAGUE klabu zitapata fedha nyingi ambapo kwa kuanza kila klabu shiriki itapata dola milioni 2.5 kwa ajili ya kusajili wachezaji na gharama za michuano kama usafiri na hotel lakini pia bingwa atapata dola za Marekani Milion 100.”