Binti wa miaka saba nchini India amemshitaki polisi baba yake mzazi baada ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyomuahidi.
Hanifa Zaara amefikisha mashtaka hayo polisi na kuwaambia kuwa baba yake amemdanganya na anatakiwa akamatwe na kushtakiwa.
Aidha, ahadi yenyewe ni ya kujengewa choo, ambapo binti huyo amesema anaona aibu kwenda kujisaidia vichakani kwa kukosa choo.
Wahindi wengi hawana vyoo na takribani watu milioni 500 huenda kujisaidia vichakani kwa mujibu wa shirika la Unicef.
“Nimekuwa nikijisikia aibu kwenda kujisaidia nje au vichakani huku watu wakiniangalia, na baba aliniahidi nikifanya vizuri darasani atanijengea choo, lakini hafanyi hivyo,”amesema Hanifa
Hata hivyo, Hanifa amabaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Ambur, jimbo la Tamil Nadu, hajawahi kuona choo nyumbani kwao.