Gnilane Diof ni mama wa mchezaji Biram Diouf amefariki akiwa kwenye hijja huko Mecca ambapo imeripotiwa zaidi ya watu 700 wamefariki.
Kutokana na wingi wa watu imekua sio rahisi kwa watu kutambulika kwasababu ya wingi wa watu hao.
Hivyo basi Mame Diouf amepata taarifa hiyo hivi karibuni.
Mama huyo alienda Mecca na dada yake Diouf ambae yeye amenusurika na kutokana na majeraha madogo madogo.
Kifo hicho kimetokana na msukumano ambao ulitokea kati ya mahujaji waliokwenda kwenye sehemu ya kuashiria kumpiga shetani mawe.
Zaidi ya ambulance 220, wafanyakazi 4000 walienda kwa ajili ya kuwasaidia watu ambao wamepata matatizo.
Hadi sasa watu walio ripotiwa kufariki ni 717 na 850 wamejaruhiwa.

Dk. Slaa Aanza Rasmi Kumpigia Kampeni Magufuli
Johan Cruyff Aukosoa Mfumo Wa Louis Van Gaal