Mmiliki wa lebo ya Cash Money Records, Bryan Williams maarufu kama Birdman ameitaja Tanzania kuwa kati ya nchi tano za Afrika atakazozitembelea mapema mwakani.

Birdman ambaye pia ni rapa, mtayarishaji wa muziki na muasisi wa lebo hiyo ameweka wazi mpango wake huo kupitia Instagram.

“Nigeria, Kenya, Tanzania, Gambia na Ghana asanteni kwa kunionesha mapenzi. Nitafanya ziara katika nchi hizo Februari 2018,” Birdman ameandika.

Birdman ambaye awali alikuwa akijulikana kama ‘Baby’ ni mmiliki wa Cash Money ambayo waliianzisha na kaka yake Ronald ‘Slim’ Williams mwaka 1991.

Cash Money imefanikiwa kuwa ngome kubwa iliyowamiliki kibiashara wasanii wakubwa akiwemo rapa Lil Wayne.

Birdman anatajwa kwenye orodha ya wasanii wa Hip Hop wenye fedha nyingi ‘Cash Kings’ akiwa na utajiri unaokadiriwa kuwa ni dola za kimarekani milioni 110 ($110 Million).

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 22, 2017
Oman kuwekeza katika viwanda vya nyama nchini